Sambaza....

Hatimae umebaki usiku mmoja pekee kuelekea katika mchezo wa Dabi kwenye Ligi namba 5 kwa ubora Barani Afrika kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya Wananchi Yanga.

Kama ilivyo ada si tu mchezo wa Ligi wa kawaida bali hubeba hisia kubwa za mashabiki wa soka nchini kutokana na umuhimu wa matokeo ya mchezo huo kwa pande zote.

Shomary Kapombe.

Kuelekea mchezo huo mbele ya Waandishi wa habari mlinzi wa kulia wa Simba Shomary Kapombe akiuzingumzia mchezo huo alisema “Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari, tumepata wiki moja ya maandalizi ambayo inatufanya tuwe tayari kwa mchezo wa kesho,” alisema na kuongeza;

“Tunafahamu mchezo wa kesho una presha kubwa na unabeba hisia kwa mashabiki na huwa unatazamwa sana sisi wachezaji tumejiandaa kwa kila kitu kuhakikisha tunashinda na kuwapa furaha mashabiki wetu.”

Robert Oliveira.

Nae kocha mkuu wa Simba Robert Oliveira ambae ameifunga Yanga mara mbili mwaka huu amesema anajua ni mchezo mgumu ambao hautabiriki lakini wamejipanga kushinda.

“Mechi ya Derby siku zote haitabiriki. Derby inaamuliwa baada ya dakika 90 za mchezo, tunaiheshimu Yanga lakini tutaingia kwenye mchezo kwa lengo la kutafuta pointi tatu.”

“Ninawaamini wachezaji wangu, wana vipaji vikubwa na tumejipanga kushinda. Sina presha ya mechi ya kesho, ni kama michezo mingine lakini kupata pointi tatu ndicho kipaumbele chetu,” alimalizia.

Sambaza....