Mechi Bora sana kuanzia mbinu mpaka uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wametupa mechi Bora sana yenye hadhi ya UEFA Champions League
4-4-2 ya Real Madrid kama kawaida yao ni kufanya Build-up kuanzia chini kupitia kwa Viungo wao wawili(Kroos & Camavinga) na kucheza pembeni zaidi kupitia kwa Runners wao(Vinicius JR, Rodrygo + Valverde ambaye alikuwa kama Free role player)!. Hapa walifanikiwa kwenye maeneo mawili…
- Kuwanyima Man City uhuru wa kukimbia kwenye nafasi pembeni zaidi hasa First Half(Foden & Bernardo wakarudi kucheza karibu sana walipo Kovacic na Rodri + Stones)
- Kuziba haraka kwa usahihi spaces ambazo Kovacic, Rodri na Stones walihitaji kupiga pasi nyuma ya Kroos na Camavinga
Man City kwenye -3-2-4-1 in Build-up hawakuwa Bora sana kipindi cha kwanza ambacho walipiga pasi nyingi ila mpinzani wao akatumia nafasi kuchukua Mchezo
Second Half Man City walirudi tofauti hasa kuja kujibu maswali ya Real Madrid
- Wafanye nini kupata nafasi pembeni?
[A]: Foden, Grealish na Bernardo lazima wakimbie kwenye nafasi kwa haraka pale tu Madrid ikipoteza mpira kwenye phase ya mwisho
[B]: Kovacic, Rodri / Stones wasipige Vertical Passes nyingi sababu muda mwingi wapo Outnumbered eneo la kiungo na badala yake wapige pembeni zaidi
- Hawapati nafasi kuingia kwenye 18 ya mpinzani wao + kupoteza Aerial Balls nyingi kupitia Haaland, Je wafanye nini kufika kwa Lunin?
[A]: Kupiga mbali zaidi ili kupata nafasi karibu na 18 sababu Real Madrid waliacha nafasi ya Man City kupiga
[B]: Kutanua uwanja ili kupita kwenye Half Spaces na Man City ipate njia eneo la katikati hakafu wapige sana kutoka mbali
Matumizi ya nafasi na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ukaamua Mchezo kuwa na magoli mengi sana Leo (Faida kubwa ni kuwa na wachezaji wengi ambao wanapiga mbali na kukimbia kwenye nafasi)
THIRD EYE. 📝
- Foden + Bernardo 🔥 usiwape nafasi ya kupiga mbele ya 18 yako 🙌
- Haaland Vs Rudiger 🔥! Jasko Gvardiol what a player 👊! Federico Valverde 🙌! Grealish 👏👏
- Vinicius JR 🧠 his Energy, Dribbling + Commitment 🔥
- RODRYGO GOES DA SILVA 🔥 TOP TOP Talent 🙌
NB: Etihad ngoma inaanza upya 😀
FT:Real Madrid 3-3 Man City, Let’s Go
Real Madrid | Stat | Man City |
14 | Shots | 12 |
5 | Shots on target | 6 |
0.63 | Expected goals | 0.86 |
38% | Possession | 62% |
423 | Passes | 690 |
11 | Fouls | 9 |
4 | Corners | 2 |
2 | Yellow cards | 2 |
0 | Red cards | 0 |
Wapwa:Anaandika @officialevodiusoscar_
Matumizi ya nafasi na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ukaamua Mchezo kuwa na magoli mengi sana Leo (Faida kubwa ni kuwa na wachezaji wengi ambao wanapiga mbali na kukimbia kwenye nafasi)
ledger app