Mashabiki wa Mnyama Simba
Stori

Simba: Si Mmejaza Uwanja? Hatutawaangusha.

Sambaza....

Hatimae ile siku ya kihistoria kwa Simba, Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla hatimae imetimia, ni leo Ijumaa ya Octoba 20 pale katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Ni uzinduzi wa michuano mipya na mikubwa ambapo Simba na Tanzania wamepewa fursa ya kufungua michuano hiyo ambapo Simba wataikaribisha Al Ahly ya Misri.

Kuelekea mchezo huo mkubwa nahodha wa Simba John Bocco amesema “Haitakuwa mechi rahisi, Al Ahly ni timu bora lakini nasi tuna timu nzuri, tuna faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu ambao watakuwa wamezaja uwanja,” alisema Bocco akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo na kuongeza:

Nahodha wa Simba Sc John Bocco.

“Kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo na tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya ili tuwe sehemu salama katika mechi ya marudiano.”

Nae kocha wa Simba Mbrazil Robertinho Oliveira amesema wanajua wanakwenda kucheza mchezo mkubwa lakini hana presha yoyote akiwa amekiandaa kikosi chake kupambana dakika 90 mbele ya wazoefu Ahly.

Robert Oliveira kocha mkuu wa Simba.

“Sina presha na mchezo wa kesho licha yakuwa ni mkubwa, hata mimi nikiwa mchezaji kule Brazil nimewahi kukutana na mechi kama hizi kwahiyo naifurahia na sina presha.”

“Ni kweli tunacheza mechi kubwa, Al Ahly ni timu bora na ina uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini mpira ni sasa na tupo tayari kwa dakika 90 za kesho,” amesema Robertinho.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x