Stori

Pesa na Kipaji? Vyote ni Muhimu.

Sambaza....

Klabu zetu zinapaswa kuwa na mfumo rafiki na mzuri wa kulinda vipaji vya wachezaji wengi ambao ni vijana na wanasajiliwa ndani ya hizi timu kubwa hapa nchini.

Vipaji ni vingi sana ambavyo unaona vinaingia ndani ya hizi klabu kubwa lakini nafasi kwao imekuwa ndogo sana! Kuna wachezaji wengi ambao waliingia klabu hizo miaka ya nyuma lakini nafasi ikawa ngumu kwao.

Denis Nkane.

Kama wakipata nafasi pia presha inakuwa kubwa sana kwenye mabega yao kupitia dakika chache wanazopata ndani ya uwanja! Tunahitaji mpango wa mafanikio wa timu zetu kipitia vipaji vya wachezaji wengi ambao wanasajiliwa.

Mfano mzuri leo hii kuhusu David Kameta “Duchu” alienda Mtibwa Sugar ambapo amecheza mechi nyingi za Ligi Kuu kwa ubora mkubwa sana hali iliyofanya yeye kurudi ndani ya Simba SC kama msaidizi wa Shomari Kapombe.

David Kameta Duchu.

Duchu ni mwakilishi wa wachezaji wengi ambao walishapita na wamesajiliwa ndani ya hizi klabu kongwe na kubwa nchini Simba na Young Africans ambao nafasi kwao imekuwa ngumu na hawapati dakika za kucheza.

Walipita kina Adam Salamba, David Bryson, Marcel Kaheza, Ally Ally, Charles Ilamfya na wengine wengi, hivi ni vipaji ambavyo vilipata wakati mdogo wa kucheza na walipopata nafasi walipokea presha kubwa sana.

Adam Salamba.

Kama ni ngumu kuwapa nafasi hawa vijana bado itakuwa ngumu kuona uwezo wao pale wakipata muda wa kucheza mechi za ushindani na mwisho wataonekana wamefeli tu sehemu husika sababu wamekaa nje muda mrefu bila kucheza.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x