Simba walipambana sana kuhakikisha wanaupata ushindi ugenini, wakaishia kupata sare ya 2-2.
Simba akicheza nyumbani, yuko na nafasi nzuri ya kusonga mbele, ikichukuliwa kuwa ni kawaida kwake kufanya vizuri katika hatua hii.
Nafasi yako Mwanakandanda kutupia utabiri wa mechi hii ujishindie Jezi ya Simba. Washindi wawili wa kwanza kutabiri watapata uzi wa Simba Sc.
Anza sasa kabla ya mechi kesho.
Simba anakuja kufa 2 mtungi hapo, nani anataka tuwekeane mzigo?
Power watatumia udhaifu walioona kwa Simba kule Zambia. Timu ilipata chances nyingi sana, lakini hazikuzaa matunda hata.
Mnyama anashinda bila mbambamba😎
Labda atashinda njaa.
Watu ambao si wa mpira tu ndio watawaza na kusema hili. Simba ni klabu ambayo kwa ukanda wetu imekomaa. Sidhani kama inaweza sahau hili licha kuwa inawachezaji wapya.
Simba haijawahi niangusha kwa Mkapa, napata tu wasiwasi huko kwa rambaramba
Mpira unadunda kaka sasa hivi ni chamanzi lolote linaweza kutokea
Simba anashinda mapema sana bila shida anatinga makundi mapema sana
Simba wanapaswa wakumbuke historia yao mbaya ya CL, huwa wanafanyaga vibayaa baaada ya msimu wa nyuma yake kufanya vyema kama ambavyo walitolewa na UD Songo na Jwaneng Galaxy
Simba 0 – 2 Power Dynamo