Ligi Kuu

Singida United kupitisha ‘fyekeo’ dirisha dogo la usajili.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Singida United kutoka mjini Singida imeweka wazi mipango yake katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa katikati ya mwezi Novemba.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Festo Richard Sanga amesema klabu hiyo haina mpango wowote wa kuongeza wachezaji katika dirisha dogo na badala yake wamekusudia kupunguza wachezaji kwani kwa sasa wanawachezaji 35.

Amesema lengo lao ni kuona klabu inabaki na wachezaji 25 hivyo kwa mantiki hiyo ni kwanza zaidi ya wachezaji 10 huenda wakaondolewa katika kikosi hicho ambacho kwa sasa ni msimu wake wa pili toka kipande ligi kuu soka Tanzania Bara.

“Nguvu kubwa tunayoelekeza ni kupunguza wachezaji, tunawachezaji 35 na tunahitaji kubaki na wachezaji 25 mpaka sasa wameshapungua wachezaji watatu hadi wanne, kwa hiyo dirisha dogo Singida United itapitisha Chujio na si kuongeza wachezaji” Sanga amesema.

Hata hivyo mbali na kupunguza wachezaji hao Singida United ambao wamekuwa na ukata wa pesa tayari wamekimbiwa na wachezaji wakiwemo wakina    Miraji Athuman, Shafik Batambuze, Peter Manyika JR na wengineyo.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x