Katika Chuji mmoja ulikua unaweza kupata viungo watatu kwa maana ya kiungo wa ulinzi, kiungo mchezeshaji na kiungo mshambuliaji, jamaa soka alilijua na lenyewe likamjua.
Haruna Moshi msimu uliopita alikua akiitumikia Yanga chini ya Mwalim Zahera kabla ya msimu kuisha na Yanga kuamua kuachana nae lakini sasa amerudi kivingine tena VPL.
Baada ya kuiondosha kwa mabao mawili kwa sifuri African Lyon katika uwanja wa Jenerali Isamuhyo Mbweni sasa KMC inasubiri mshindi kati ya Kagera Sugar ama Azam f c ili kucheza nae nusu fainali.