Mo Dewji alipowasili uwanja wa Mkapa tayari kabisa kufanya mahojiano na vyombo mbambali vya habari
Uhamisho

Mo Dewji: Fiston Mayele Anaweza Kuja Simba.

Sambaza....

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohamed Dewj “Mo” amesema hana shida yoyote endapo Fiston Mayele ataangukia Msimbazi na kuvunja mkataba na Wananchi Yanga.

Mo akizungumza na mwandishi nguli wa habari nchi Saleh Jembe amesema hamafahamu vizuri Fiston Mayele kwani huwa haangalii mechi za Yanga lakini anajua ni mchezaji mzuri.

 

“Kwa bahati mbaya huwa sifwatiliagi mechi za Yanga lakini huwa namsikiaga na namuona kwenye mitandao ya kijamii akifunga magoli ni mchezaji mzuri na namuombea kila lakheri afanikiwe,” alisema Mohamed Dewji

Kuhusu kumsajili Mayele Simba Mohamed Dewji amesema hajui mkataba wake na Yanga upoje lakini kama benchi la ufundi Simba watamtaka na yeye mwenyewe atakua tayari basi anakaribishwa Simba.

Fiston Mayele.

Mohamed Dewji “Sijui mkataba wake na Yanga upoje unajua sisi Simba ni klabu kubwa hivyo tunahitaji mchezaji yoyote yule mzuri lakini kwasasa sijui hali yake ya mkataba na Yanga labda kama ataamua kuvunja mkataba nao.

Lakini pia ili yote hayo yatokee ni lazima kwa upande wetu tukubaliane, lazima scouts na benchi la ufundi wakubaliane hilo. Na hiyo si tu kwayeye (Mayele) hata kwa wachezaji wengine Afrika ni lazima apitishwe na benchi la ufundi,” alimalizia Mo

Kwasasa Fiston Mayele ndie kinara wa ufungaji mabao katika Ligi kuu ya NBC akiwa na mabao 15 akiwakimbiza nyota wa Simba Moses Phiri (10), Saidoo Ntibazonkiza (10) na John Bocco mwenye mabao 9.

Sambaza....