ASFC

Hawa hapa wababe wa FA, Championship wamekaza.

Sambaza....

Mwishoni mwa wiki iliyopita michuano ya kombe la FA maarufu kama AzamSports Federation Cup iliendea nchini katika viwanja mbalimbali kama ambavyo ratiba ilivyopangwa tangu awali.

Baada ya michezo 32 kupigwa hatimae timu 16 zimepatikana na kufuzu hatua hiyo ya 16 Bora huku bingwa mtetezi wa kombe hilo Yanga ikiwa timu yamwisho kufuzu hatua hiyo.

Katika timu 16 zilizofuzu kuna timu 11 kutoka Ligi Kuu ya NBC, timu 4 kutoka Ligi ya Championship na timu moja kutoka Ligi ya mkoa.

Kutoka Ligi ya Championship ambayo imetoa timu nne ambazo ni  Green Worriers, JKT Tanzania, Pan Africans zote za Dar es salaam na African Sports ya Tanga.

Baadhi ya michezo ya 16 ni pamoja na Simba dhidi ya African Sports, Yanga dhidi ya Tanzania Prisons na Azam Fc dhidi ya Mapinduzi Fc pia Kagera Sugar atavaana na Mbeya City.

Sambaza....