Sambaza....

Anaitwa Levran Lima Pereira maarufu kama Pepe

Alizaliwa na kukulia chini Brazil lakini alitimkia Ureno akiwa na umri wa miaka 18

Mwaka 2006, baba yake mzazi alisema kuwa amepigiwa simu na kocha wa timu ya taifa ya Brazil akimuhitaji Pepe kikosini lakini mchezaji huyo alikataa na kuamua kuichezea Ureno

Image result for pepe brazil

Alipojiunga na Real Madrid akitokea Porto kwa ada ya euro milioni 30 mwaka 2007 aliweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kwenye La liga

Alikuwa nyota wa mchezo wa fainali ya euro 2016 dhidi ya Ufaransa na alichaguliwa kwenye kikosi bora cha michuano hiyo

Aliwahi kugombana na José mourinho wakati huo akiwa kocha wa Real Madrid kutokana na kitendo cha kocha huyo kumweka benchi aliyekuwa kipa tegemeo wa Madrid wakati huo, Iker casillas

Image result for pepe and mourinho

Pepe ni mume wa mrembo na muigizaji maarufu nchini Ureno, Ana moreira na wawili hao wana watoto wawili wa kike ambao ni Angeli na Emily

Kwa kipindi cha miaka 10 akiwa real madrid aliicheza mechi 334 akiipa mataji matatu ya la liga, matatu ya ligi ya mabingwa ulaya na mawili ya kombe la mfalme

Pepe amejikusanyia kadi za njano 79 na nyekundu 5 na ni michezo 49 pekee aliingia akitokea benchi tangu asajiliwe Madrid

Pepe ana kadi nyekundu nyingi.

Pepe alikuwa akihusika sana katika matukio yenye utata ya el classico lakini kubwa zaidi ni lile la kumuumiza beki wa Barc Dani alves

Ingawa mkataba wake na Besiktas haujawekwa wazi lakini imeelezwa kuwa moja vipengele vinaweka wazi msahara wake wa euro milioni 3.25 kwa mwaka


Sambaza....