Ligi Kuu

Hiki ndicho kilicho mpa Tshishimbi ubabe wa Februari

Sambaza....

Kiungo mahiri wa Yanga sc, Papy Tshitshimbi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa mwezi Februari 2018

Mchezaji huyo raia wa Congo (DRC) ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda kiungo mwingine wa Yanga sc, Pius Buswita na mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda Emanuel Arnold Okwi

Kwa mwezi Februari Okwi aliongoza kwa kufunga mabao, baada ya kufunga mabao 4 akifuatiwa na Tshishimbi aliyafunga mabao 3 huku Pius Buswita akifunga mawili, lakini Tshishimbi akiwa na pasi moja ya bao pia kwenye michezo ya mwezi huo akuoneshwa kadi yoyote, huku Okwi akioneshwa kadi ya njano

Pia kingine kilichofanya Tshishimbi kutwa tuzo ni kuiwezesha Yanga sc, kukusanya alama 12, kwa mwezi Februari, wakati Simba sc ilikusanya alama 10 tu

Kwa kutwaa tuzo hiyo, Tshishimbi atazawadiwa fedha shilingi za Tanzania milioni moja, kutoka kwa wadhamini wa ligi kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, pamoja na kisimbuzi kutoka kwa wadhamini wa matangazo Azam TV na ngao maalum ya ushindi huo

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x