Sambaza....

Kocha msaidizi wa Mwadui FC, Jumanne Ntambi, amefariki dunia usiku wa leo baada ya kuanguka bafuni akiwa anakoga nyumbani kwake mkoani Shinyanga

Taarifa zinasema mara baada ya kuanguka kocha Ntambi alikimbizwa hospitali ambako walipofika walisema tayari ameshafariki

Ntambi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na hivi karibuni alikwenda hospitali na kushauliwa apumzike na jana aliwatembelea wachezaji wa Mwadui wakati wa mazoezi kwenye uwanja wa Mwadui complex

Marehemu Jumanne Ntambi ni mzaliwa wa Musoma mkoani Mara, ingawa inaelezwa kuwa familia yake inaishi Moshi mkoani Kilimanjaro

Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi “Amin”

Sambaza....