Ligi Kuu

Kwenye mechi hii Yanga anaonekana kama kondoo aliyelala

Sambaza....

Hapana shaka kesho ni sikukuu ya Simba na Yanga, sikukuu ambayo husimamisha shughuli zote zinazofanyika hapa nchini kwa masaa kadhaa.

Mitaa yote hupendezeshwa na bendera za timu hizi mbili, rangi za njano, kijani, nyekundu na nyeupe hutamaraki machoni penu.

Hii yote ni kuonesha kuwa timu hizi zinamashabiki wengi kila kona ya nchi hii ndiyo maana kila nafsi, kila jicho na kila sikio hutamani kusikia matokeo ya mechi hii.

Tambo huwa zinakuwa nyingi sana, kila shabiki hujinasibu yeye ni bora zaidi ƴya mwezake ili mradi tu kumnyong’onyesha mpinzani wake.

Yanga kwenye mechi hii wanaonekana wanyonge sana. Simba inaonekana ina matokeo mazuri kuzidi Yanga kwa sasa, haijapoteza hata mechi moja mpaka sasa hivi na ikiwa inaongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 58 na Yanga ikiwa na alama 47.

Nafasi ya Simba na Yanga katika msimamo

PosTimuPWDLGDPts
11951334418265443
21881264220194420
31911055036148365
4183556563-16230
5182556067-35225

Simba inatofauti kubwa ƴya magoli ya kufunga na kufungwa , mpaka sasa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni magoli 45 wakati Yanga tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni magoli 27.

Hii inaonesha jinsi gani ambavyo Simba wana safu imara ya ulinzi na ya kushambulia kuliko Yanga na inafaa kusema Simba wanaingia kwenye mechi hii wakionekana ni bora zaidi ya Yanga.

Yanga wamekuwa na matatizo mengi sana msimu huu kama wachezaji wake wengi nyota kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Na matatizo mengi ya ukata yanayoongelewa mpaka kusababisha kocha wao mkuu George Lwandamina kuwakimbia.

Hii yote inaonesha kuwa Yanga ni kondoo aliyelala, hakuna anayemfikiria hata mara moja kuwa anaweza akafanya kitu chenye madhara kwenye vita hii.

Ni wapole sana , hawaongei sana na hawajigambi sana ukilinganisha na wenzao hutokosea utakaposema kuwa hawajiamini kuelekea kwenye mechi hii.

Hapana shaka wanaingia kama “underdogs” kwenye mechi hii, hii itakuwa na faida kwao au hasara kwao kutokana na wao watakavyolichukulia jambo hii la wao kuwa underdogs.

Faida kwao ya kuwa underdogs itakuja pale watakapokubali ana na hali halisi kuwa wao ni underdogs na kucheza mpira bila presha ya aina yoyote kama timu ambayo haina cha kupoteza chochote.

Kukubalia kwao kuwa underdogs kutawafanya wacheze kwa umakini na kufanya maamuzi kwa utulivu mkubwa.

Utulivu ukiwa ndani yao hawatakuwa na makosa mengi binafsi ndani yao hivo watakuwa na nidhamu ya matumizi ya kila nafasi ambayo watakuwa wanaipata.

Utulivu huu utawapa shida pia Simba kwa sababu itawafanya wao wacheze katika presha ya juu kwa sababu watajiona wao siyo “underdogs” na presha kubwa ya kupata matokeo itakuwa ndani yao kwa sababu washajiona wao siyo underdogs, hapa umakini utakuwa mdogo ndani yao kwa sababu watakuwa na presha kubwa ndani yao.

Hasara ƴya Yanga kuwa “underdogs” itakuja kipindi ambacho hawatakubaliana n na hii hali ya wao kuwa underdogs kwa sababu uoga utakuwa ndani yao.

Watacheza bila kujiamini na kuwafanya wacheze bila utulivu na kufanya maamuzi ambayo yatakuwa hayana faida kwenye timu kwa sababu ya kukosa utulivu ndani yao.

Hizo ndizo faida na hasara za Yanga kuwa underdogs kwenye mechi hii. Simba wanatakiwa waingia katika presha ya kawaida, presha ambayo itawafanya wao wasijiamini sana.

Wawe katika hali ya kawaida, hali ambayo itaongeza utulivu mkubwa katika kufanya kwao maamuzi ndani ya mchezo huu.

Kila mtu anaiangalia Simba kama timu ambayo itashinda mechi hii, ni timu ambayo itapata matokeo kwa sababu ya kiwango chao bora na kwa sababu ya haja yao kubwa ya kushinda ubingwa msimu huu.

Wana miaka 5 hawajafanikiwa kushinda ubingwa wa ligi kuu na hii mechi inaonekana ni mechi ambayo itawahakikishia wao kushinda ligi msimu huu. Kwa hiyo presha kubwa itakuwa kwao kuanzia kwa mashabiki mpaka wachezaji , hivo wakiruhushu presha hii iwe kubwa mpaka kwa uwanjani wana nafasi kubwa ya kupoteza mchezo huu

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x