Jonas Mkude
Tahariri

Lazima Mkude Aende Ili Kutengeneza Simba Mpya.

Sambaza....

Kuna baadhi ya majina walioagwa ni kutokana na kutofikia matarajio hao inaeleweka vyema sana na hakuna anayepinga kisha kuna majina ya ”Seniors” kama Erasto Nyoni na Jonas Mkude hawa sio “issue” ya kiwango bali wanapisha zama mpya ndani ya Simba.

Kile kizazi chao ni sehemu ya mafanikio makubwa ya Simba na wametwaa karibia kila kitu ndani hivyo sasa ni rasmi imefikia tamati na taratibu wanapaswa kuondoka! Simba haiwezi kuwatoa wote pamoja ila nina uhakika madirisha makubwa mawili yajayo wote huenda watakuwa wametoka.

Hii ni kawaida kwa klabu yoyote ya mpira ile “cycle” ikiisha hakuna namna unaweza kumtuma tena mchezaji akafanye kitu na hakuna namna mchezaji anaweza kujipush kufanya kitu, ni time ambayo klabu na mchezaji wanapaswa kupeana changamoto mpya sehemu nyingine.

Jonas mkude akimnyanyasa kiungo wa Al-Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Real Madrid kile kizazi chao cha UEFA tatu mfululizo, hawakuondoka wote bali mmoja mmoja ama wawili kwa madirisha manne na hatimae wote hawapo! Nawaelewa Viongozi wa Simba na “with time” Simba itakuwa na sura nyingi mpya kwa ajili ya zama mpya.

Ushauri wangu, kwenye zama zao hawa wakina Nyoni, Mkude na wengine klabu ichukue wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuwasomesha masuala ya utawala wa mpira, wengine ukocha na wengine Scouting! Hii itakuja kuwa faida kubwa sana kwa klabu kwakuwa hiki ndio kizazi ambacho kilipata “exposure” na “experience” zaidi kwenye historia ya Simba kuliko chochote.

Klabu ione namna watapomaliza “career” zao rasmi basi wapambane kuwarejesha kisha waje kuitumikia Simba kama Maofisa wa klabu kwenye vitengo mbalimbali, unaweza kumpa Mkude Jonas kama Balozi wa Simba (Official Club Ambassador) ambaye ataiwakilisha Simba kwenye majukumu mbalimbali mfano huko CAF ambapo klabu hutuma watu kama Jonas kwenye tuzo.

Erasto Edward Nyoni.

Unaweza kumpa nafasi mtu kama Nyoni kuwa Mshauri wa Rais au nyota mwingine yoyote wa zama zao, ambaye ni “real football talk” na Rais wa heshima ama Mwenyekiti wa Bodi, ile damu ya mpira ikaingia ama mmoja akateuliwa kama Mjumbe wa bodi kwakuwa wameuishi sana mpira wa miguu.

Farhan Jnr.

Sambaza....