Sambaza....

Mabingwa wa kombe la mapinduzi Azam FC, imeshindwa kuonesha cheche zake baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Lipuli FC katika mchezo wa ligi kuu bara

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Samora mjini Iringa, ulikuwa na ushindani mkubwa kwa dakika zote tisini

Kwa matokeao hayo yanaifanya Azam kujikusanyia alama moja, na kufikisha alama 35, baada ya kushuka dimbani mara 19, ikiendelea kusalia nafasi ya tatu ikizidiwa kwa alama mbili na mabingwa watetezi Yanga wanaoshika nafasi ya pili huku vinara Simba SC wakiwa na alama 42

Lipuli FC wanapanda hadi nafasi ya saba wakifikisha alama 20 baada ya michezo 19, na kuzishusha timu za Ruvu shooting na Mbao lakini zenyewe zinamchezo mmoja mkononi

Aidha ligi hiyo inataraji kuendelea tena kesho kwa mchezo miwili kupigwa ambapo Kagera sugar wataikaribisha Singida United kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Kagera huku Njombe mji FC ikiikaribisha Majimaji FC kunako dimba la sabasaba mjini Njombe

Sambaza....