Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba, Masoud Juma.
Tetesi

Masoud Djuma anarudi kuungana na Matola…

Sambaza kwa marafiki....

Habari za chini ya kapeti zilizotua katika meza ya Uhamisho ya Kandanda.co.tz   ni kocha msaidizi wa zamani wa klabu ya Simba Sc, Masoud Djuma, anaelekea kujiunga na klabu ya KMC kuchukua nafasi ya Etienne.

Ni leo (07/06) tu KMC walithibitisha kuwa Etienne hataendelea na mkataba katika klabu hiyo itakayoshiriki Kombe la Shirikisho maimu ujao, hii inawezekana kuwa kuna nafasi ya Djuma kuwa mfalme wa KMC msimu ujao.

Matola

Kwa upande wa Seleman Matola, naye inasemekana anakuja kuungana na Masoud katika kuisuka kiushindani klabu hiyo yenye makazi yake wilayani Kinondoni, jijini Dar es slaaam.

Zaidi tutawaletea kwa undani..

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.