Blog

Mrisho Ngassa naye kuikimbia YANGA

Sambaza....

Baada ya wimbi la wachezaji wengi wa Yanga kuondoka katika klabu hiyo yenye masikani yake Kariakoo katika mitaa ya jangwani kutokana na ukata unaoikabili timu hiyo.

Wachezaji kadhaa wameahaachana na timu hii Baada ya kutolipwa mishahara Yao ya miezi miwili iliyopita. Mpaka sasa hivi klabu hiyo imeshaachana na Sadney, Juma Balinya.

Na mwanzoni iliripotiwa baadhi ya wachezaji kuandika barua ya kuondoka kwenye klabu hiyo. Wachezaji hao ni Issa Birgimina , Lamine Moro , David Molinga. Leo hii katika ukurasa wa Instagram wa Mrisho Ngassa inaonesha na yeye anaonekana kuachana na Yanga.

Mrisho Ngassa ameandika maneno ambayo yanaleta maswali mengi kwa watu wengi , ambapo kupitia ukurasa wake ameandika kuwa “ukiwa unakula na kipofu usimshike mkono, Always Next time tutaonana tena Mungu akipenda”.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.