Stori

Simba: Kwa Mkude Swala Lilikua ni Muda.

Sambaza....

Baada ya kutangaza kuachana na Jonas Mkude baada ya miaka 12 msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally ametoa yamoyoni yeye binafsi akimuelezea mchezaji huyo akizungumzia muda ndio umewatenganisha.

Ahmed Ally akiandika katika ukurasa wake wa instagram amesema “Ameondoka mtu tunaempenda kweli, ameondoka mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu. Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda,” alisema Ahmed.

Kwa miaka kadhaa wakati anaitumikia Simba Jonas alikua akihusishwa na kutakiwa na vilabu vya Azam na Yanga lakini haikua hivyo kwa Jonas hakuwahi kuiacha Simba.

Jonas Mkude (kulia) akiitumikia Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Nkana

“Wakati Simba ina njaa, Azam ilimhitaji hakuenda, akachagua kuvumilia njaa yetu huyu ni zaidi ya mchezaji kwetu. Sisi tulitamani Jonas Mkude amalizie mpira wake Simba kwani hatutaki kucheza nae akiwa timu nyingine. Kwa sababu tukimfunga ataumia na yeye akitufunga ataumia hatuko tayari kumuumiza Mkude wetu.”

“Tumetoa taarifa ya kuachana nae punde tutatoa taarifa ya kumuaga na tutamuaga kwa heshima zote. Sisi ndo tunatambua zaidi heshima ya Mkude kuliko mtu mwingine yeyote na tutamuaga kwa heshima hii.”

Sambaza....