Ligi Kuu

Yanga sc yapandisha mzuka, sasa ni mpaka kieleweke

Sambaza....

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Yanga sc, jioni ya leo wameendeleza ubabe wao baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga.

Katika mchezo huo, uliofanyika kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Yanga waliandika bao la kwanza baada beki wa Stand Ally Ally kujifunga dakika ya 8 ya mchezo huo akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na Yusuf Mhilu.

Tano Bora

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC30209162154769
2Azam FC301610435161958
3Yanga SC301410644232152
4Tanzania Prisons30121262722548
5Singida Utd FC30111183028244

Dakika chache baadae Yanga waliandika bao la pili kupitia kwa kiungo wake wa ushambulizi Ibrahim Ajib, akimalizia kazi nzuri ya kiungo kinda Maka Edward, na hadi timu zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao hayo 2-0.

Kipindi cha pili Stand United inayonolea na kocha Almas Niyongabo, ilionekana kubadilika sana na kuishambulia Yanga kama nyuki kabla ya kupata bao dakika ya 82, kupitia kwa Tariq Seif akiunganisha klosi ya Vitalis Mayanga.

Obrey Chirwa aliihakikishia Yanga ushindi baada kufunga bao la tatu, likiwa ni bao lake la 12 msimu huu, kunako dakika ya 84, baada ya kumpiga chenga beki wa Stand na kufumua shuti kali lililomshinda kipa wa Stand.

Ushindi huo, unaifanya Yanga sc kufikisha alama 46, ikilingana na mahasimu wao Simba lakini zikitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Simba ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Yanga iliwakilishwa na Youth Rostand, Juma Abdul, Gadier Michael, Said Juma “Makapu”, Kelvin Yondan “Cotton”, Maka Edward, Yusuf Mhilu, Pius Buswita, Obrey Chirwa, Raphael Daud/ Juma Mahadhi dk74, na Ibrahim Ajib/ Emmanuel Martin dk75

Stand United Mohammed, Aron Lulambo, Miraji Maka/ Makenzi Kapinga dk78, Ally Ally, Erick Mulilo, Jisend Mathias/ Ismaily Gambo dk66, Bigirimana Blaise, Abdul Swamad/ Sixtus Sabilo dk80, Tariq Seif, Ndikumana Suleiman na Vitalis Mayanga.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x