Shirikisho Afrika

Yanga imetangulia na Simba itafuata!

Sambaza....

Kikosi cha Yanga kimeondoka alfajiri ya leo kuelekea nchini Mali kuelekea katika mchezo wao wa tatu katika kundi wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga baada ya kumaliza mchezo kwa ushindi dhidi ya KMC katika Ligi ya NBC ililazimika kurudi kambini na kujiandaa na safari  ya kuelekea nchini Mali kwenda kuvaana na Real Bamako wenye alama moja katika kundi D. Mpaka sasa Yanga wana alama tatu wakishika nafasi ya pili nyuma ya US Monastier wenye alama nne. 

Yanga wanakwenda ugenini wakiwa wanajiamini baada ya kuibamiza TP Mazembe mabao matatu kwa moja na hivyo kurudisha matumaini yakufuzu robo fainali ya michuano hiyo yapili kwa ukubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Pia kwa upande wa watani zao Simba wao wanatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kuelekea nchini Uganda kuvaana na Vipers katika Dimba la St. Mary. Simba na Vipers ndio vibonde katika kundi lao kwani wote wawili hawajapata ushindi mpaka sasa.

Katika msimamo wa kundi D Simba wanashika nafasi yamwisho wakiwa nyuma ya Raja (mwenye alama 6) Horoya (alama 4) na Vipers wenye alama moja pekee.

Simba si tu hawana alama lakini pia hawajafunga bao lolote mpaka sasa katika michuano hiyo hivyo mchezo wa Vipers unatarajiwa kuwa mgumu na wakufufua matumaini yao yakufuzu robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Sambaza....