Mabingwa Afrika

CAF yazidi kuikalia kimya Simba

Sambaza....

Barua ya Simba bado haijajibiwa na CAF kuhusu mwamuzi kubadilishwa. Awali mwamuzi ambaye alipangwa kuchezesha mechi hiyo alikuwa anatoka Ethiopia.

Lakini ghafla CAF walibadilisha mwamuzi na kumpa mwamuzi kutoka Ndola nchini Zambia kwa sababu ambazo zinaelezewa ni za kiufundi.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio hapa nchini Mkuregenzi mtendaji wa Simba amedai kuwa wao Simba hawalalamiki kwa hofu ya kuonewa.

Ila wanacholalamika ni kutopewa sababu nzito kwanini mwamuzi kabadilishwa ghafla kwa sababu ambazo hazijaanishwa vizuri.

Mkurugenzi huyo mtendaji wa Simba alizidi kuelezea kuwa Ndola mpaka Lubumbushi ni eneo la karibu ,unaweza kutumia masaa mawili au matatu kufika Lubumbashi.

Hivo kuna uwezekano kunaweza kufanyika kwa mchezo mchafu ambao unaweza kuifanya Simba ihujumiwe kwenye hii mechi.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x