Chama x Baleke, Simba Sc
Mabingwa Afrika

Wataweza Kwelii!?

Sambaza....

Hakuna jambo gumu ukijaribu, hakuna lisilowezekana ukifanya. Asiyejaribu kufanya chochote hatapata chochote. Wahenga walisema “Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu” wakimaanisha ukitafuta na kupambana hutakosa chochote.

Lakini swali la msingi hapa ni, Je utaweza kupata chochote? Utafanyaje ikiwa mazingira ni magumu? Vipi kama utakosa nafasi ya kufanya chochote ?

 

Mchezo wa mkondo wa kwanza wa mechi za mtoano kati ya Power Dynamos ya Zambia dhidi ya Simba ya Tanzania ulimalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili katika dimba la Levy Mwanawasa pale Ndola Zambia.

Mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi Septemba na mwanzoni mwa Oktoba ambapo mchezo huu wa matuadiano baina ya Simba dhidi ya Power Dynamos utapigwa jijini Dar es salaam katika viunga vya Azam complex.

Katika mchezo wa kwanza pale Ndola Zambia timu zote zilicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi, lakini Simba walitengeneza nafasi nyingi zaidi lakini hawakuzitumia vema kiasi cha kushindwa kuumaliza mchezo wakiwa ugenini.

Clatous Chama akipiga mpira kufunga bao mbele ya mlinzi wa Power Dynamos.

Mshindi wa jumla katika michezo yote miwili atavuka na kwenda moja kwa moja katika hatua ya makundi. Je ni Simba au Power Dyanoms ambaye ataibuka mshindi katika mchezo wa marudiano ? Ukizingatia ushindi wowote kwa timu yoyote utaibeba.

Sare tasa au sare ya bao moja kwa moja utaibeba Simba kwa faida ya goli la ugenini, sare pacha ya magoli mawili kwa mawili utaufanya mchezo uende katika mikwaju ya penati kwani kutakuwa na uwiano sawa wa magoli ya nyumbani na ugenini kwa timu zote mbili, sare yoyote ya kuanzia magoli matatu na kuendelea kutaibeba timu wageni kwa faida ya goli la ugenini.

Wachezaji wa Simba Pape Sakho na Clatous Chama wakishangilia moja ya magoli yao katika mchezo dhidi ya Horoya ambapo Mnyama alishinda 7-0!

Simba amekuwa na rekodi nzuri sana katika michezo ya Kimataifa hususani wakiwa nyumbani, katika michezo ya Ligi ya mabingwa wakiwa nyumbani wamecheza michezo 19, Simba wamepoteza michezo miwili, huku wakitoa sare michezo mitatu na kushinda michezo 14, na katika jumla ya michezo hiyo wamefunga magoli 41 na kuruhusu magoli 11 pekee ya hivi karibuni.

Michezo ambayo Simba walipoteza ni ule dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa msimu wa 2021/22 ambapo Simba walibamizwa magoli matatu kwa moja wakiwa nyumbani kufuatiwa na mchezo wa kwanza ambao walishinda magoli mawili kwa bila wakiwa ugenini na kutolewa katika mashindano kwa faida ya goli la ugenini.

Kotei (Kushoto) akimthibiti Muleka wa TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao uliisha kwa sare.

Lakini pia katika msimu uliopita Simba ilichapwa mabao matatu kwa bila na Raja Casablanca katika hatua ya makundi. Mechi walizotoka sare ni dhidi ya Tp Mazembe msimu wa 2018/19, kisha UD Songo msimu wa 2019/20 katika hatua za awali kisha sare dhidi ya Plateau Utd ya Nigeria msimu wa 2020/21.

Simba akiwa katika uwanja wa nyumbani huwa tofauti sana kwani timu vigogo wa Afrika walipigika akiwemo Al ahly ya Misri, Wydad Casablanca, Kaizer Chiefs, Orlando Pirates na vigogo wengine wengi. Je, Power Dynamos atauweza mfupa huu walioushindwa mafisi? Ukizingatia toka msimu wa mwaka 2011 Power Dynamos hawakuwahi kuvuka hatua hii na kuingia makundi.

Kibu Denis na Jean Baleke wakishangilia bao pekee katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa.

Kwa takwimu hizi Power Dynamos kuitoa Simba akiwa nyumbani lbda itokee tuuh. Lakini pia swali la msingi ni, Je Simba wataweza kuiendeleza rekodi hii ya kibabe? Je wakali hawa wa Msimbazi wataendeleza undava wao wakiwa nyumbani?

Lakini Usisahau mpita una matokeo ya kushangaza, mpira una matokeo matatu yaani sare, ushindi au kupoteza, lolote linawezekana kwenye mpira, chochote kinaweza kutokea katika soka.

NB: NGOJA TUONE.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x