Na tayari muitikio mkubwa umeonekana huku baadhi ya mashirika na watu binafsi wakinunua tiketi 100 mpaka 300 kwa wakati mmoja ilo zigawiwe kwa wanawake wataokwenda katika mchezo huo.
Yanga wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi yakufuzu robo fainali kwani kusuasua kwa Mazembe kumezidi kuwapa nafasi katika kundi hilo ambalo US Monastir anaonekana ndio mbabe
Kwa hesabu zozote zile leo Yanga hawapaswi kupoteza mchezo kama itashindikana alama tatu basi angalau wapate alama moja ili kuendelea kuweka hai matumaini yao ya kufuzu robo fainalo
Simba si tu hawana alama lakini pia hawajafunga bao lolote mpaka sasa katika michuano hiyo hivyo mchezo wa Vipers unatarajiwa kuwa mgumu na wakufufua matumaini yao yakufuzu robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika.
wachezaji wazuri ndio chachu ya mafanikio katika klabu lakini Mazembe kwa sasa ina wachezaji wazuri wasiozidi watano ambao wanaweza kucheza katika klabu zetu hapa Tanzania.
Katika zoezi hilo alikuepo Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe ambae hakusita kuwaita Wananchi siku ya Jumapili ili kuwashangilia wachezaji wao na kuiteketeza TP Mazembe.