Ligi Kuu

Mayele: Ni mchezo muhimu tumejiandaa vyema.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Geita Gold ambao utapigwa leo katika Dimba la Azam Complex Chamanzi nyota wa Yanga wamesema wapo tayari na wamejiandaa kwa mchezo mgumu dhidi yao.

Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga na nyota wa Timu ya Taifa ya Congo DR amesema wanakwenda kuingia katika mchezo mgumu na muhimu kwao kama Yanga.

 

“Ni mchezo muhimu kwetu na tunahitaji kupata pointi tatu mashabiki wetu wawe mapoja nasi. Tupo tayari kwa mchezo ambao utakua na ushindani mkubwa, Geita Gold dhidi yetu Yanga mchezo haujawahi kuwa rahisi hivyo tutajitahidi kusaka ushindi,” Fiston Mayele

Yanga wanaingia katika mchezo huo utakaopigwa saa moja usiku wakiwa kileleni huku pia wakiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Geita kwani katika mchezo wa raundi ya kwanza waliibuka na ushindi wa bao moja bila lililofungwa na Benard Morrison.

Baada ya ushindi wa jana wa Simba na kufikisha alama 57 huku Yanga akiwa na alama 62 ni wazi sasa alama za uongozi kwa Yanga zimebaki 5 pekee hivyo ni muhimu kwao kushinda leo ili kuendeleza alama nyingi katika uongozi wao.

Huu ni mchezo pekee wa Yanga katika Ligi kwa mwezi Machi kwani baada ya mchezo huu watakwenda katika majukumu ya Kimataifa na baada ya hapo kupisha mapumziko kwa mechi za Kimataifa.

Sambaza....