Ligi Kuu

Msemaji Simba: Mambo ni magumu!

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Alli amekiri msimu huu ni ngumu wao kutwaa ubingwa kutokana na aina ya matokeo wanayoyapata katika Ligi.

Ahmed Ally amekiri mambo ni magumu na kitendo cha kutoka sare dhidi ya Azam kinazidi kuwapa wakati mgumu na kuwapa faida Yanga.

“Tunaendelea kumpa faida mpinzani wetu na asilimia kubwa zipo kwake, tunaendelea kupambana lakini mambo ni magumu na kila Mwanasimba anatakiwa kuelewa hivyo kwasasa.” Ahmed Ally.

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Alli.

Mpaka sasa Yanga wapo kileleni wakiongoza Ligi kwa tofauti ya alama 10, wakiwa na alama 60 wakati Simba wana alama 50 nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kituo kinachofwata kwa Simba ni Mwanza katika dimba la CCM Kirumba katika mchezo dhidi ya Geita Gold.

Sambaza....