Salum abubacar akimiliki mpira katikati mwa viungi wa Simba Thadeo Lwanga na Mzamiru Yassin
ASFC

Simba na Yanga kurudi tena uwanjani March

Sambaza....

Michuano ya kombe la FA maarufu kama Azamsports Federation Cup litaendelea tena kutimua vumbi mwezi March mwaka huu katika raundi ya nne.

Katika raundi hiyo Simba ndio watakua wakwanza kuingia uwanjani ambapo watawakaribisha African Sports “Wanakimanumanu” kutoka Tanga, mchezo huo utapigwa March mbili katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Feisal Salum wa Yanga

Mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga Sc wao watakua Kwa Mkapa March tatu kuwakaribisha Tanzania Prisons. Huku pia siku hiyo kutakua na mchezo mwingine ambapo Geita Gold watakua wenyeji wa Green Worries.

March nne kutakua na michezo mitatu ambayo ni Ihefu dhidi ya Pan Afrika, Mtibwa Sugar dhidi ya KMC na Singida Big Stars dhidi ya JKT Tanzania kutoka Ligi ya Championship.

Michezo ya mwisho ya kuhitimisha raundi hiyo ya nne itapigwa March tano ambapo Azam Fc atawakaribisha Mapinduzi Fc na Kagera Sugar dhidi ya Mbeya City.

Baada ya raundi hiyo ya nne kumalizika washindi wote watakaopata ushindi na kuvuka watakutana robo fainali ya michuano hiyo.

Sambaza....