Wakati Julio anakabidhiwa timu zilikua zimesalia mechi nne na moja ya lengo alilopewa na kuinusuru timu isishuke daraja na angalau ikaangulie kwenye playoffs wakajiulize.
Nitoe rai kwa mashabiki wote wa KMC na wakazi wa Kinondoni kwamba bado tuna nafasi yakwenda kupambana mpaka tone la mwisho, ni kipindi ambacho tunahitaji kutumika zaidi ili msimu unaokuja tuweze kuwepo
KMC FC itakaporejea mbali na kukutana na Geita Gold Aprili 17 , pia itakuwa na kibarua kingine dhidi ya Dodoma Jiji, Singida Bigi stars, Tanzania Prisons pamoja na Mbeya City
Kwaupande wake Nahodha wa KMC FC Sadalah Lipangile amesema kama wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo huo huku akiwasihi mashabiki kutokukata tamaa kwasababu bado wana nafasi ya kufanya vizuri