Usajili wa Simba unaonekana kuwa ni wa kimikakati zaidi, hasa kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu na madhaifu yaliyojitokeza katika kikosi kwa msimu ujao kuanzia kwenye ligi hadi klabu bingwa Afrika.
Bwalya amejiunga na Simba akitokea kwao Zambia katika klabu ya Lusaka Dynamos, ambapo inasemekana Simba waliwapokonya wenzao Yanga tonge mdomoni kutokana na Yanga pia walimuweka kwenye mipango yao ya usajili katika msimu huu.