Ligi Kuu

Timu NNE za kuzikamia msimu huu

Sambaza....

Kwa mara ya kwanza mtandao wa kandanda ulitoa tuzo kwa Timu Galacha ya Msimu 2019/20, ambayo itafahamika kama G’chaa Oyee au Galacha Oyee, tuzo hii ilienda kwa klabu ya Simba Sc.

Haikuwa bahati mbaya Simba kutwaa tuzo hii, kwa misimu mitatu iliyopita klabu hii imekuwa na matokeo mazuri zaidi na kufanikiwa kutwaa kombe la Ligi Kuu Tanzania bara Mara tatu. Lakini, hii haitoshi, Simba ilikuwa na matokeo mazuri dhidi ya timu ngumu katika ligi hii.

1. Kwa upande wa mtandao wetu kutwaa ubingwa pekee haikuwa kigezo cha kutwaa Tuzo ya Timu Galacha ya Msimu, tuliangalia vitu vifuatavyo vigezo hivi.
Timu NNE katika msimu wa 2019/20 ndicho kwanza kilikuwa kigezo cha awali, tukiangalia kutumia takwimu zetu.

2. Pia tukaangalia rekodi ya timu hizo top-four zilikuwa na matokeo gani katika msimu huo dhidi ya timu NNE bora kwa misimu mitatu iliyopita hii ukiwa pamoja na msimu wa 2019/20 kwa misimu mitatu iliyopita.

Kwanini tumefanya hivyo, kuanzia msimu wa 2017/18 mtandao huu umekusanya takwimu ambazo tunaamini watumiaji ni wataalamu wa kiufundi katika vilabu na timu ya Taifa. Ukiwa na lengo la kuwawezesha kutumia takwimu hizi katika kupanga jinsi ya kupambana na timu pinzani katika msimu husika au ujao.

Hizi ndio timu ukikutana nazo hakikisha unashinda msimu huu

Hivyo basi, unagundua kuwa timu ili iwe Timu Galacha ya Msimu ni lazima ijihakikishie kupata alama na matokeo mazuri dhidi ya vilabu ambavyo vimejikusanyia alama nyingi kwa msimu husika, na Kandanda ni jibu la hayo maswali.

Tuzo yetu ukiwa miongoni mwa vikombe vya Simba. (Picha: Simba Sc)

Klabu ya Simba inaweza kuwa nanafasi nzuri kutwaa tena tuzo hii msimu huu, lakini pia itatakiwa kuzingatia matokeo na ‘giants’ wa misimu mitatu iliyopita. Kandanda itaendelea kukusanya taarifa muhimu ili kufanikisha hili.

Tunawakaribisha pia wadau na wadhamini mbalimbali ambao wanaweza kutuongezea thamani tuzo hii na iendelee kuwa chachu ya matokeo ya uwanjani na malengo ya kiushindani kwa vilabu vyetu kwa maslahi ya soka la Tanzania.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.