Moja ya mikutano ambavyo timu inaweza kutangaza viingilio au utaratibu wa mapato yao. Pichani ni Haji Manara, Msemaji wa Simba SC.
Ligi Kuu

Manara: Mwamuzi alikua hovyo!

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara amemzungumzia mwamuzi wa mchezo wao wa jana kati ya klabu yake Simba na Ihefu na kusema huenda angeongelewa kuliko hata mchezo wa Yanga na Prisons uliofanyika jijini Dar es salaam.

Manara ameamua kusema hayo baada ya mwamuzi wa mchezo huo kukataa magoli mawili halali kwa timu zote mbili kwa kusema wafungaji walikua wameotea.

“Mwamuzi msaidizi huyu Lau asingekataa hili goli halali “angetrend” sana jana usiku na leo angeweza kuwa maarufu kuliko sare ya kwa Mkapa jana.

Ndio, tayari alishawanyima Ihefu goli linalofanana na hilo kabla na mjadala ungekuwa Simba imebebwa Mbeya lakini sasa stori ni mshika kibendera avurunda Sokoine Stadium.” Hajji Manara.

Manara pia alizungumzia uhalali wa waamuzi kuchezesha mchezo bila kujali kutaka kusawazisha makosa, lakini pia uhalali wakutoa maamuzi bila kujali ukubwa wa timu.

“Maamuzi yake mawili ni ya hovyo ila yanabeba dhana kuu ya baadhi ya waamuzi wetu ya kupenda “kubalance” mambo uwanjani.

Yaan kwa kuwa baadae aliona alikosea kuwanyima goli halali Ihefu ni lazima arudishie na kwa Simba, yaani kukosea mara mbili au tatu na hata mara kumi kwao haina shida ili mradi.”
Msemaji huyo wa klabu ya Simba amesema wakati mwingine waamuzi wanashindwa kutoa hata penati mbili katika mchezo mmoja wakihofia kuoenekana kuibeba timu moja.
“Ndio maana Bongo siku hizi huwezi kukuta mwamuzi katoa penati zaidi ya moja au mbili kwa timu moja katika mechi kwa kuogopa ataonekana anaibeba timu hata kama ni kweli wapinzani wametenda madhambi yanayostahili hizo penati.
“Na ikitokea katoa penati basi hiyo timu iliyopewa iwe makini, anaweza kufanya makosa nje kidogo ya eneo la hatari, refa akafunika kuwa penati na pia mchezaji wao anaweza kufanya kosa linalostahili  kadi ya njano lakini mwamuzi akatoa kadi nyekundu ya moja kwa moja.”

Sambaza....