Simba itatangaza ubingwa katika mechi dhidi ya Ndanda, uwanja wa taifa au dhidi ya Singida United pale Namfua, lakini hayo yote yatakuja endapo Yanga atashinda mechi zake zote za ligi.
Kwa sasa Sevilla ipo chini ya mwalimu Joaquin Caparros, wakiwa na nyota mbalimbali wanaowategemea kama Ben Yedder mwenye mabao 17 na nahodha wao Ever Banega.
Ilikuwa Simba wacheze na Yanga ili kufahamu nani atacheza na Sevilla lakini baada ya kuangalia mambo kadhaa wamekubaliana na SportPesa kuwa Simba ndio wanaopaswa kucheza na timu hiyo kutoka Uhispania.