Mirambo amesema kuna orodha ndefu ya makocha ambao wanaitaka kazi hiyo, na Ettiene ni mojawapo wa watu wanaoangaliwa na Shirikisho ili kupata nafasi hiyo.
Kutakuwa na makundi 10, kundi letu litakuwa na timu nne, tutacheza mechi 6, tatu ugenini na tatu nyumbani. Mechi hizi zinahitaji mbinu za uwanjani na hata nje ya uwanja. Waokota mipira ni sehemu ya mashambulizi na ulinzi wa Stars.
Harambee vs Stars ni mechi ya ‘Afrika Mashariki’ na si mechi ya marudio ya zile nyingi ambazo wameshakutana, ni ‘vita’ , vita hasa ya kwenda kutengeneza rekodi mpya kwa kila timu kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.