Harakati za usajili katika klabu ya Yanga zinaendelea kwa kasi kubwa, baada ya msimu uliomalizika kuwa na kikosi hafifu Yanga wanapigana ili wawe na kikosi ambacho ni imara.
Taarifa ambazo tovuti yetu imezipata ni kwamba kilichomkwamisha Ajibu kwenda TP Mazembe ni biashara ambayo imefanywa kati ya Ajibu na Simba kabla ya ofa ya TP Mazembe kutua mezani kwa klabu ya Yanga.
Kutoa zaidi ya milioni 80 kwa mchezaji kama Ajib sawa, lakini je, mchezaji huyo ataongeza ubora gani mpya katika safu ya washambuliaji kama John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.?