Kuachwa kwa wachezaji hawa ‘mastaa vijana’ kutoka klabu kubwa nchini za Simba na Yanga kunapaswa kuwafumbua zaidi kimchezo vijana hao kama kweli wanataka kufikia malengo yao makubwa.
Mshambuliaji huyo makini wa Ndanda, huenda alikuwa katika orodha ya majina ambayo Mwinyi Zahera aliacha wakati akiondoka kwenda kuungana na kikosi cha timu ya taifa ya Congo.