Timu ikiwa na mdhamini katika usafiri, inapunguza gharama.
Blog

Wadau wanaelekea kuinunulia basi Lipuli Fc

Sambaza....

Katika kile kinachoonekana ni katika kupunguza kero za klabu ya Lipuli Fc. Mashabiki na wadau wa timu hiyo kutoka mkoani Iringa wamejiwekea malengo ya kununua basi la timu ifikapo mwezi Agosti.

Vilabu vingi katika Ligi kuu vinapitia changamoto nyingi ikiwemo fedha za kujiendesha. Hata klabu kikubwa kama Yanga kilianzisha kampeni yake ya kuchangia timu kutoka kwa wanachama na wapenzi wake. Hivyo kwa hiki kinachofanywa na Lipuli si Kigeni na si cha aajabu.

Kandanda ilijaribu kupata ukweli wa jambo hili kutoka kwa viongozi wa kundi la wadau lililoanzisha mchakato huu. Walituhakikishia mchakato huo ni wa wadau na mashabiki wake ndio wameuanzisha na viongozi wote wanafunga mkono kwa asilimia mia kabisa, na wanaendelea kuwahamasisha wadau wengine kutoa ahadi au kuchangia pia.

Kwa upande wa chama cha mpira wa miguu cha mkoa wa Iringa, IRFA, Kupitia Mwenyekiti wake bwana Cyprian Kuyava nao wameonekana kuunga mkono juhudi hii na kupelekea yeye kama yeye kutoa ahadi ya shilingi milioni moja.

“Huu ni mchakato mzuri na ofisi yetu kama chama cha mpira wa miguu mkoa, tunaunga mkono jitihada zote zinazolenga kuboresha soka letu. Lipuli kama mwakilishi wa mkoa pia anahitaji nguvu za wadau wote wanaoguswa” Bwana Kuyava aliiambia tovuti ya Kandanda.co.tz. Mwenyekiti ambaye amekuwa nguzo muhimu katika soka la mkoa wa Iringa.

Wadau hao wameshakusanya ahadi kiasi cha zaidi ya milioni 10 hadi sasa.

Nani atamiliki basi hilo?


Kwakuwa basi hilo limechangiwa na wadau, mmiliki wa basi hilo itakuwa ni Lipuli Fc na ndio watakuwa wamiliki wa nyaraka zote muhimu kuhusu basi hilo.

Itatatua changamoto?


Wachezaji wa Lipuli wakiwa kwenye moja ya safari zao.

Kwa kiasi kikubwa ndio, kwa sababu kwa sasa Lipuli inatumia basi la kukodi aina ya Coaster ambalo ni dogo  na kama likipatikana kubwa litawanufaisha zaidi na kuweza kusafiri nalo popote.

Mafuta na Huduma nyingine?


Ni wakati mwafaka sasa wa makampuni pia kuipa sapoti Lipuli katika sehemu ya usafiri huu kama utapatikana ili basi liweze kusafiri. Hii inaweza kuwa kwa kuweka mafuta na huduma zinazohusiana. Na mdhamini pia naweza kuweka matangazo yake katika basi hilo popote liendapo. Au kwakuwa hili halijanunuliwa na mdhamini huyo linaweza kuwa na tangazo dogo tu ili kutokuharibu nembo ya Lipuli lisalo tu ‘Fueled by ……’ na kuweka logo tu za wadhamini wake wote.

Mfano wa basi la Lipuli Fc

Unataka kuwaunga mkono?

Kwa wadau wengine, Taasisi au Makampuni yanayotaka kuunga mkono mchakato huu unaweza kuwasiliana na waratibu wa mchakato huu Bwana Michael Mlowe, namba yake ni +255 655 149 840 au Bwana Abousufiani Sillia +255 713 446 699

Tuziunge mkono juhudi za wadau zinaanzishwa kwaajili ya kuziletea maendeleo klabu zetu katika ngazi zote.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x