Okwi na magoli tisa katika michezo mitano Oktoba.
BAADA ya kuanza msimu kwa mwendo wa chini, mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Mganda, Emmanuel Okwi ameanza kuwasha moto wake mwezi huu baada ya kufunga magoli saba- ikiwemo ´HatTrick´ katika michezo mitatu iliyopita ya Simba SC. Okwi ilimlazimu kusubiri hadi mchezo wa mzunguko wa saba kufunga...