Sambaza....

Mabingwa wa kombe la mapinduzj klabu ya soka ya Azam FC, leo hii imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya, katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara

Katika mchezo huo ambao Azam FC, walikuwa ugenini kunako uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya

Haikuwa kazi nyepesi kwa Azam FC kuweza kuibuka na ushindi huo, kwani ilibidi wasubiri mpaka kunako dakika ya 70, ndipo mlinzi wake Yakub Mohammed alipoifungia bao la kwanza

Tano Bora ya Ligi Kuu Bara

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2041404618401122279466
2Yanga SC1961334320326117209442
3Azam FC1981105038301148153380
4Kagera Sugar FC198596871168204-36245
5Tanzania Prisons196577267171190-19243

Wakati Prisons wakiendelea kutafakari namna ya kupata bao la kusawazisha, walijikuta wakifungwa bao la pili likiwekwa kimiani na mshambuliaji Paul Peter kunako dakika ya 83

Kwa ushindi huo waliopata Azam FC, unawafanya kufikisha alama 30, na kuwasogeza mpaka nafasi kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wakiishusha Simba SC yanye alama 29, lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambapo kesho watakuwa ugenini kuikabili Kagera Sugar

Sambaza....