Ligi Kuu

CAF huenda wakaitembelea Tanzania

Sambaza....

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF litafanya ukaguzi wa mfumo wa leseni kwa vilabu kwenye upande wa miundo mbinu

Caf wakankusudia kufanya ukaguzi huo, wa kutembelea na kutazama miundo mbinu ili kuhakikisha mfumo huo unatekelezeka ipasavyo kwa kuanzia na mtazamo wa vigezo vya miundo mbinu

Wakati wa miaka kadhaa ya kuzindua mfumo huo wa leseni kwa vilabu, changamoto kubwa kunako bara la Afrika imeonekana ni vigezo vya miundo mbinu ambavyo kwenye baadhi ya viwanja vinavyotumika wakati wa mashindano vimekuwa vikitoa taswira isiyo nzuri kwa mashindano ya CAF

Kwa mwaka huu wa 2018, wameandaa ukaguzi huo utakaohusisha vilabu vyote vitakavyoshiriki hatua ya makundi kwenye mashindano ya vilabu ya CAF, wakielekeza kwenye viwango na ubora wa viwanja vya kuchezea mechi na vile vya mazoezi

Tayari shirikisho hilo linepanga kuchagua kundi la wakaguzi, watakakwenda kwenye klabu ya kila mwanachama wake ili kukusanya ripoti itakayowasilishwa, na moja kati ya ripoti hiyo ni miundo mbinu ya uwanja itakayothibitisha kama uwanja umefidhi mahitaji ya kutumika kwa mechi za CAF

Viwanja ambavyo havitakidhi mahitaji hayo havitaidhinishwa kutumika kwa mashindano na havitatumika kwa mchezo wowote wa hatua ya makundi kwa mashindano ya vilabu kwa mwaka huu wa 2018

Kwa uamuzi huo, huenda CAF wakaitembelea Tanzania endapo vilabu vya Simba na Yanga vitafudhu kwenye hatua ya makundi ya michuano ya shirikisho hilo, ambapo Sumba SC watashiriki kunako kombe la shirikisho huku ndugu zao Yanga SC wakishiriki kwenye michuano ya vilabu bingwa barani Afrika (Ligi ya mabingwa)

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x