EPL

EPL

Emery: Tunaikaribia ndoo ya Ubingwa.

Baada ya sare ya bao 1-1 na kiwango mujarabu dhidi ya Liverpool jana usiku, kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery amesema wamekaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu England. Emery amekitaja kiwango ambacho wamekuwa wakikionesha kama ni uthibitisho wa kuwa bora na kuimarika tofauti na mwanzoni mwa ligi walipoitwa majina mengi....
EPL

Mmiliki wa Leicester City afariki dunia.

Mwaka 2016 Vichai Srivaddhanaprabha na familia nzima ya Leceister City walitupatia mashabiki wa soka muujiza ambao hautajirudia tena miaka ya karibuni. Tutawakumbuka daima, baada ya Leicester City kuchukua ubingwa wa dunia akiwa na kikosi cha gharama ndogo. Mungu azilaze pema peponi roho za wote waliokuepo kwenye ajali ya Helicopter iliyotokea...
EPLUhamisho

David de Gea mlango uko wazi

Kwa mara ya kwanza, Jose Mourinho, kocha wa Manchester United, amekiri kuwa ana wasiwasi David Degea hataweza kuongeza mkataba wake wa kuitumikia Manchester United, imeripotiwa. Mkataba wa Degea unaisha katika majira ya joto, na katika mkataba huo kuna kifungu kinachoiruhusu Man Utd kumuongezea mkataba wa hadi miezi 12. Degea toka...
EPL

Alonso aongeza mkataba Chelsea.

Beki kutoka nchini Hispania na klabu ya Chelsea Marcos Alonso amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya mgharibi mwa jijini London. Alonso mwenye umri wa miaka 27, amekamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya, ambao utamuweka Stamford Bridge hadi mwaka 2023, na ni dhahir unavunja tetesi za kuondoka kwake mwishoni...
EPL

Cascarino: Kocha Sarri hajui kumtumia N’Golo Kante.

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Tony Cascarino ameonesha kuchukizwa na mfumo wa meneja wa sasa wa klabu hiyo Maurizio Sarri, kwa kusema haumpi nafasi kiungo kutoka nchini Ufaransa N'Golo Kante, kucheza kama ilivyokua misimu miwili iliyopita. Cascarino ambaye aliitumikia Chelsea kuanzia mwaka 1992–1994 na kufunga mabao manane katika michezo...
EPL

Mesut Ozil ajimwagia sifa baada ya kuwaadhibu Leicester City.

Kiungo wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil amejisifia kwa kuonesha soka safi usiku wa kuamkia leo, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Leicester City, waliokubali bakora tatu kwa moja, kwenye uwanja wa Emirates jijini London. Ozil ambaye jana alikua nahodha wa kikosi cha The...
EPL

Tottenham yapata Pigo.

Klabu ya Tottenham Hotspur imezidi kupata pigo baada ya kuripotiwa kuwa kiungo raia wa Kenya Victor Wanyama anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo kutokana na kuumia msuli wa paja wakati akiitumikia timu yake ya Taifa. Wanyama ambaye aliiongoza Kenya hapo jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-0...
EPL

Manchester United kumuongezea Mkataba Luke Shaw.

Klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza imekubali kumuongeza mkataba beki wake wa kushoto Luke Shaw ambaye mkataba wake wa awali unakaribia kufikia kikomo mwezi Julai mwakani. Taarifa zimesema Shaw mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuongeza mkataba mrefu na mnono zaidi kuliko ule wa awali aliosaini mwaka 2014...
EPL

Spurs kutumia uwanja wao mpya mwezi Disemba.

Kikosi cha Tottenham Hotspur kina matumani ya kurejea kwenye uwanja wa White Hart Lane Disemba 26 mwaka huu, tayari kwa mapambano ya ligi kuu ya soka nchini England pamoja na michuano ya kimataifa. Taarifa zilizothibitishwa na uongozi wa klabu hiyo zinaeleza kuwa, uwanja wa White Hart Lane ambao umefanyiwa maboresho...
1 6 7 8 9 10 15
Page 8 of 15