Idadi kubwa ya magoli ligi kuu Tanzania bara anayo yeye, yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote, anagoli zaidi ya 100. Mchezaji aliyezifunga goli nyingi timu za Simba na Yanga rekodi pia anayo yeye. Ni mchezaji bora wa msimu uliopita. Na ni kepteni wa timu kubwa kama Simba. Bado unamchukulia poa tu?.
Tabiri matokeo kwa kuandika katika sehemu ya maoni ndani ya tovuti yetu tu ya mechi hiii. Mtu wa kwanza kuwa sahihi kabla ya mchezo kuanza atajipatia tiketi ya VIP B mechi ya Simba SC vs AS V.Club na Jezi ya Klabu ya Simba.
Ugumu wa mechi ya Simba vs As Club Vita utachagizwa na matokeo ya mechi za awali yaani Simba dhidi ya JS Saoura na AS Vita dhidi ya Al ahly. Jumla AS Club Vita wanaweza kupata alama 1-3 katika michezo yake miwili iliyosalia na mwisho wa siku kuwa na jumla ya alama 5-7.