Uhamisho

Gabr atua West Bromwich Albion

Sambaza....

Klabu ya West Bromwich Albion imethibitisha kumsainisha mkataba wa mkopo beki Ali Gabr wa Zamalek ya Misri mpaka mwishoni mwa msimu huu

West Bromwich Albion imetangaza usajili huo kupitia tovuti yake, na ikieleza kuwa Gabr ataungana na raia mwenzake wa Misri Ahmed Hegaz kwenye safu yao ya ulinzi

“Ni mchezaji ambaye tulikuwa tukimfatilia kwa muda tangu kwenye fainali za mataifa ya Afrika ambapo walikuwa wakicheza pamoja na Hegaz” alisema mkurugenzi wa ufundi Nick Hammond

“Tuliendelea kumfatilia zaidi na tukaona huu ni wakati muafaka kwetu kumchukua mchezaji huyo” aliongeza Hammond

Aidha klabu hiyo, bado inaendelea na harakati zake za kujiimalisha kabla dirisha la usajili kufungwa siku ya Jumatano, tayari imeonesha dhamira ya kumchukuwa nahodha wa Watford Troy Deeney

Meneja wa klabu hiyo, Alain Pardew, tayari emetenga kitita cha pauni milioni 18, kumnunua Deeney huku ikielezwa pia amekukuwa akimuhitaji Daniel Sturridge kwa mkopo kutoka kunako klabu ya Liverpool

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x