Ligi Kuu

Hizi ndizo tofauti kati ya Simba na Yanga msimu huu.

Sambaza....

Msimu umemalizika, msimu ambao tumeshuhudia Simba ikibeba kombe kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano huku Yanga akipoteza ubingwa wake baada ya kuchukua kwa mara ya tatu mfululizo, zifuatazo ni tofauti ambazo zilionekana kati ya Simba na Yanga msimu huu.

1: Kipa vs Golikipa

Yanga walikuwa na kipa wakati Simba walikuwa na Golikipa, Aishi Manula alihakikisha analinda goli la Simba kwa kuhakikisha anakuwa kiongozi kwa kuipanga safu yake ya ulinzi ili isiwe na makosa mengi ambayo yangesababisha Simba kufungwa magoli mengi ya uzembe. Kikubwa zaidi alifanikiwa kupata cleansheets 18 hii ilitoa tafasri halisi ya neno golikipa kwani aliwekeza muda wake kulinda goli.

Wakati huohuo Youthe Rostand alitumia muda mwingi kuwa kipa wa Yanga, alikuwa mmoja ya wachezaji ambao walikuwa wanakamilisha idadi ya wachezaji wa Yanga. Hakuwa na msaada maradufu kwenye kikosi chake kwani makosa mengi binafsi yalikuwa yametawala kwenye gloves zake, hata akili yake ilikosa uwezo wa kuwaongoza mabeki wake ambao walikuwa wanafanya makosa mengi binafsi.

2: Tunaamini golikipa ndiye beki wa kwanza na ndiye mshambuliaji wa kwanza, chochote kile ambacho kitafanywa kimakosa na gloves zake kitakuwa na nguvu kubwa ya kubomoa morali ya wachezaji kupigana, na siku zote safu imara ya ulinzi hukamilika kipindi ambacho kipa na mabeki wake kuwa imara, kitu hiki kilionekana kwa Simba kwani walikuwa na safu imara ya ulinzi kuzidi Yanga. Simba waliruhusu magoli 15 na Yanga waliruhusu magoli 20.

3: Sifa moja ya wanajeshi vitani ni kujilinda na kushambulia kwa pamoja, kwao wao hawana kipa, beki na mshambuliaji, wote huwa najukumu moja kulingana na wakati husika, kitu hiki kilionekana katika jeshi la msimbazi. Mabeki wa Simba walikuwa msaada mkubwa sana katika upatikanaji wa magoli kwa mfano Erasto Nyoni ametoa pasi nane (8) za magoli, Asante Kwasi alifunga magoli matatu (3) baada ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili, Shiza Kichuya alifunga magoli saba(7) na kutoa pasi za nwisho zaidi ya kumi tano, kuna alama kubwa inayotenganisha “team work” ya Simba na Yanga msimu huu.

4: Waliumia sana baada ya kukosa ubingwa kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, hawakuendelea kulia kwa sababu ya tatizo lililowatokea. Umuhimu wa kukarabati nyumba yao ulikuwepo katika akili yao, wakafanya kila walichokiamini kitapendezesha nyumba yao, wakaleta mabati imara kutoka kwa Aishi Manula yaliyoezekwa kwenye ukuta imara wa sementi ya kina Erasto Nyoni, wakaona kuna umuhimu wa kutumia rangi ya kampuni la Shomari Kapombe, rangi ambayo ni kiraka , ukiraka ambao ulitumika ipasavyo kwenye masika na kiangazi na msingi wa magoli imara yalioimarisha timu yalitoka kwenye miamba ya kina Emmanuel Okwi na John Bocco mwisho wa siku timu ikawa na uwiano mzuri katika eneo la kujizuia na kushambulia mpaka ikawa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa arobaini na saba (47) huku Yanga wakipata tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ishirini na moja (21).

5: Inawezekana wingi magoli ambayo yalifungwa na Yanga msimu uliopita yalihamia katika kikosi cha Simba, Simba ilihitaji wachezaji wawili tu kuonesha uhai wa safu ya ushambuliaji, wachezaji ambao walihusika katika magoli zaidi ya 35 wao wawili. Bila shaka John Bocco na Emmanuel Okwi walikuwa mhimili mkubwa katika safu ya ushambuliaji, na Yanga walikosa watu mhimili katika safu yao ya ushambuliaji na ndiyo maana hata kipindi ambacho timu ilihitaji nguvu za mtu mmoja kuibeba mtu huyo alikosekana.

6: Joseph Omong na George Lwandamina walianza pamoja msimu mpya lakini wote hawakumaliza msimu huu. Waliondoka , lakini kuondoka kwao kulitofautiana, yupo aliyeondoka na timu haikutetereka sana na mwingine aliondoka na timu ikaanguka. Wakati Joseph Omong anaondoka nafasi yake kwa mara ya kwanza ilichukuliwa na Masoud Djuma, kocha bora wa ligi kuu ya Rwanda na baadaye akaja Pierre Lenchantre na Joseph Omong aliondoka katikati ya ligi tena kipindi ambaco ligi ilikuqa kwenye mapumziko hali ambayo ilimpa Simba uwezo wa kujipanga lakini kwa Yanga kulikuwa na picha tofauti, George Lwandamina aliondoka kipindi ambacho ligi ilikuwa imebakiza mechi chache kumalizika hivo hawakuwa na muda wa kujipanga, hata watu ambao walichukua nafasi yake hawakuwa na uwezo mkubwa pamoja na uzoefu mkubwa wa kuisaidia Yanga.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x