Nasradinne Nabi katika kikao cha Waandishi wa Habari katika moja ya michezo ya Shirikisho Afrika.
Shirikisho Afrika

Kocha Yanga: Tulichopata Nigeria Hakina Maana Tena

Sambaza....

Wananchi Yanga kesho watakua dimbani kuwakaribisha Rivers United katika mchezo wa raundi ya pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United.

Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Yanga Nasradine Nabi amesema matokeo ya mchezo wakwanza yatakua hayana Maana kama hawatakata tiketi ya nusu fainali.

“Wachezaji wote wako vizuri na wanajituma mazoezini na kwa pamoja tunajua bado hatujafuzu tunahitaji matokeo mazuri kesho ili tuweze kwenda hatua inayofuata,” alisema Nabi na kuongeza

“Nimekaa na wachezaji wangu na tumekubaliana kuwa kazi nzuri tuliyoifanya Nigeria itakua haina maana kama hatutashinda mchezo wa kesho.”

Zawadi Mauya.

Kiungo wa Yanga Zawadi Mauya akiongea kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema wao hawatazami mchezo mmoja pekee bali watapambana mpaka mwisho ndio wataangalia walichokipata.

Zawadi Mauya “Tunajua tunakwenda katika mchezo utakaoandisha historia ya klabu yetu, sisi wachezaji lengo letu ni moja tuu kuvuka hapa na kwenda mbali zaidi. Mwishoni ndio tutaangalia ni historia gani tumeweka lakini sio sasa hivi.”

Yanga watakua uwanja wa Benjamin Mkapa kesho saa moja usiku kuwakaribisha Rivers United huku wakiingia na mtaji wa mabao mawili kwa sifuri walioupata katika mchezo wakwanza ugenini.

Sambaza....