Wachezaji wote wako vizuri na wanajituma mazoezini na kwa pamoja tunajua bado hatujafuzu tunahitaji matokeo mazuri kesho ili tuweze kwenda hatua inayofuata,
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika bila timu yoyote kupata goli na ikamlazimu kocha wa Yanga sc kufanya mabadiliko mwanzoni tu mwa kipindi cha pili
Nae kiungo wa pembeni wa Yanga Benard Morrison akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema hawakwenda Nigeria kujifurahisha wanataka kushinda mchezo huo
Ninaelewa kuwa Young Africans imeijenga upya timu yake na wanafanya vizuri wakati huu kwenye ligi ya ndani, pia wameongoza kundi lao kwenye kombe la shirikisho
Wananchi wana kila sababu yakuandika historia mpya yakutinga nusu fainali ya michuano ya Shirkisho Afrika kutokana na kikosi walichonacho lakini pia faida ya kuanzia ugenini.
Kuelekea mchezo huo Yanga imeondoka na kikosi chake chote cha wachezaji tegemeo huku wakiwaacha nchini nyota wake wachache kwasababu mbalimbali ikiwepo majeruhi na sababu za kiufundi.