NYOTA wa Manchester City Sergio Kun Aguero, ameeleza kwamba ataondoka klabuni hapo mwaka 2020 na kurejea kunako klabu ya nyumbani kwao.
Aguero mwenye miaka 29, amebakiza misimu miwili tu kutimka katika Ligi kuu ya England.
Muargentina huyo amesema atarejea kunako timu ya Independiente, ambapo ndio ilimtoa kabla ya kujiunga na Atletico Madrid.
“Mkataba wangu na Manchester City utakufa mwaka 2020, kisha nitarudi nyumbani kwaajili ya kuichezea Independiente,” alisema Aguero.
Kun Aguero ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Manchester city mpaka sasa. Akiwa amefunga magoli 143 kwenye michezo 204 aliyoitumikia City.
Tayari Aguero ameshinda mataji mawili ya Ligi kuu England akiwa na Man City, na yupo mbioni kushinda taji la tatu akiwa chini ya kocha Pep Guardiola.