Blog

Licha ya kesi ya Ubakaji, Ronaldo atajwa tuzo za Ballon d’Or.

Sambaza....

Mshambuliaji wa Juventus na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amejumuhishwa kwenye majina ya awali ya wachezaji 10 ambao watawania tuzo ya mchezaji bora wa dunia za Ballon d’Or inayotolewa na Jarida maalumu la Ufaransa.

Ronaldo ambaye ameshinda tuzo mbili zilizopita na tuzo tano kwa ujumla wake sawa na Mshambuliaji wa Argentina na Barcelona Lionel ambaye anatazamiwa kuonekana katika majina mengine 20 kukamilisha idadi ya majina 30 yanayotarajiwa kutajwa ili kupigiwa kura.

Kutajwa kwa Ronaldo kunakuja siku chache baada ya kutajwa kuhusika na tukio la ubakaji la mwaka 2009 la mwanadada Kathryn Mayorga huko Las Vegas marekani, na tayari Klabu yake ya sasa Juventus na makampuni kadhaa yakiwemo Nike na Eletronic Arst Inc wakitangaza kuifuatilia kwa karibu kesi hiyo.

Aidha tuzo hii awali ilikuwa ikisimamiwa kwa pamoja na FIFA toka mwaka 2010 hadi 2015 kabla ya FIFA kuanzisha tuzo zake ambazo toka mwaka 2016 Cristiano Ronaldo ameshinda mara mbili na mwaka huu imekwenda kwa kiungo Luka Modric.

Majina 10 ya awali:

Sergio Aguero (Argentina, Manchester City)

Alisson Becker (Brazil, Liverpool)

Gareth Bale (Wales, Real Madrid)

Karim Benzema (France, Real Madrid)

Edinson Cavani (Uruguay, Paris St Germain)

Thibaut Courtois (Belgium, Real Madrid)

Cristiano Ronaldo (Portugal, Juventus)

Kevin De Bruyne (Belgium, Manchester City)

Roberto Firmino (Brazil, Liverpool)

Diego Godin (Uruguay, Atletico Madrid)

Kandanda itakuletea majini mengine 20 pindi yatakapotangazwa kufikisha idadi ya wachezaji 10, pamoja na Vipengele vingine.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x