Mabingwa Ulaya

Liverpool yaichinja Roma, Salah, Mane na Firminho waweka rekodi zao

Sambaza....

Liverpool wameendeleza dhamira yao ya kuhakikisha wanashinda kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, baada ya kuichapa As Roma kwa mabao 5-2 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa kunako dimba la Anfield jijini Liverpool, Uingereza

Shujaa wa Liverpool alikuwa ni Mohammed Salah, aliyefunga mara mbili kabla ya kutengeneza mabao mengine mawili na Liverpool kuanza kuchungulia fainali ya michuano hiyo

Wachezaji wa As Roma wakiwa hoi na Mziki wa Liverpool

Roberto Firminho pia amefunga mabao mawili, huku mshambuliaji Msenegali Sadio Mane akifunga bao moja na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga

Hii inakuwa mara ya 8 kwa Sadio Mane, Roberto Firminho na Mohammed Salah wote kufunga katika mchezo mmoja.

Firminho akishangilia bao

Pia mabao mawili aliyofunga Salah yanamfanya kufikisha idadi ya mabao 43, akiwa na Liverpool msimu huu akifukuzia rekodi ya Ian Rush ya msimu wa mwaka 1983/84 ambapo alifunga mabao 47, kwa msimu

Mashabiki wakiwa na furaha tele

Mabao mawili alifunga Firminho anafikisha idadi ya 10, na kuifikia rekodi ya ufungaji wa idadi hiyo katika michezo michache, Adriano alifunga mabao 10 katika michezo 11.

Mane pia hakukosekana kwenye orodha ya wafungaji.

Edin Dzeko na Diego Peroti waliifungia Roma mabao mawili, na kufufua matumaini pengine wanaweza kubadili matokeo katika mchezo wa marejeano utakaofanyika kunako dimba la Estadio Olympico jijini Roma, Italia

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x