Sambaza....

Kamati ya maadili ya Shirikisho la soka nchini (TFF) inakutana leo Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala la makamu wa rais wa TFF, Michael Richard Wambura aliyefikishwa kwenye kamati  akituhumiwa kwa makosa matau ya kimaadili

Akidaiwa kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kughushi barua na kushusha hadhi ya shirikisho hilo

Taarifa iliyotolewa leo na TFF, kwa vyombo vya habari nchini imeeleza kuwa Wambura amefikishwa kunako kamati ya maadili kwa makosa matatu

Aidha taarifa hiyo haikumtaja mtu aliyemfikisha kunako kamati hiyo kwa makosa hayo, pia taarifa hiyo imefafanua kuwa makosa hayo yote ni kinyume cha kifungu cha 73(1), 73(7) za Kanuni za maadili za TFF toleo la 2013 na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF 2015

Sambaza....