
Klabu ya Mbeya city fc, imefanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi kutokana na uhitaji na nafasi; mabadiliko haya yanahusisha nafasi ya Kocha Msaidizi, Meneja wa Timu na Mtunza vifaa.
Mwalimu Mohamed Kijuso amerejea katika timu yake ya awali (Timu B) na ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo yenye nyota wachanga. Timu hii ya vijana imekua lishe kwa timu kubwa na tuna imani itasaidia kuongeza ushindani katika kikosi chetu. Mwalimu Josiah Steven ambaye ndiye kocha wa magolikipa wa Mbeya City FC anakaimu nafasi ya Kocha msaidizi.
Godfrey Katepa aliyekua meneja wa timu na Rashid Kasiga aliyekua mtunza vifaa wa klabu, wamemaliza mikataba yao na klabu yetu. Klabu itatangaza watumishi watakaochukua nafasi zao.
Unaweza soma hizi pia..
Azam kujimaliza yenyewe mbele ya Simba!
Miongoni mwa maeneo yatakayopa ushindi Simba katika mchezo huo ni eneo la kiungo na eneo la mlinda mlango.
Kola tishio jipya kwa Onyango na Inonga
Hazikupita siku nyingi Mayele akakutana na Simba na kutiwa mfukoni na Mcongo mwenzake Inonga Baka na kupeleka kuzima mtetemo wake
Mbinu mpya za Yanga zilizoacha lawama kwa kipa wa Dodoma Jiji
Nasredeen Nabi ilimlazimu kutoka katika mfumo wake wa siku zote wa kumtegemea Fiston Mayele na kubadili mbinu ili kupata ushindi.
Kipa Dodoma katolewa tuu kafara!
Ndani ya miaka miwili unataka kuniambia ameisha kabisa? Je hatupaswi kumshukia kocha wake wa makipa?