Sambaza....

Meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Thomas Tuchel, amejitokeza hadharani baada ya kusema kwamba yupo tayari kuchukua nafasi ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger pindi akiachana na timu hiyo.

Ripoti kamili inaeleza kwamba kocha huyo wa zamani wa Dortmund, amepeleka ombi lake la kuhitaji kuifundisha Arsenal wakati ambapo Wenger atakapo achana na Arsenal.

Tuchel mwenye umri wa miaka 44, awali tayari alifuatwa na Bayern Munich kwaajili ya kumrithi Jupp Heynckes mwishoni mwa msimu huu lakini yeye hakuonyesha utayari juu ya hilo, badala yake aliihitaji Arsenal.

Kocha huyo aliifundisha Dortmund kwa muda wa misimu miwili na alifanikiwa kuipatia ubingwa klabu hiyo.

Tuchel, pia ameripotiwa kuwindwa vikali na vilabu vya Paris St-Germain ya Ufaransa na Chelsea ya Uingereza, vikionesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Sambaza....